Madini yaingiza shilingi milioni 924.7 wilayani Kakonko

DODOMA-Imeelezwa kuwa, katika kipindi cha kuanzia mwaka 2019 hadi 2023 jumla ya shilingi 924,685,884 zilikusanywa kutokana na madini yaliyozalishwa katika Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma.
Hayo yamesemwa leo Agosti 30, 2024 na Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa alipokuwa akijibu swali lililoulizwa na Mhe. Aloyce John,Mbunge wa Buyungu aliyetaka kujua kiasi cha fedha zilipopatikana kutokana na madini katika Wilaya ya Kakonko kuanzia mwaka 2019 hadi 2023.

Akijibu swali, Dkt. Kiruswa amesema kuwa, Wilaya ya Kakonko ni miongoni mwa Wilaya zilizojaliwa kuwa na madini ya dhahabu nchini.

"Kutokana na madini yanayozalishwa Kakonko Shilingi 725,171,133.52 zilitokana na mrabaha na Shilingi 199,514,750.46 zilitokana na ada ya ukaguzi wa madini yaliyozalishwa kwa kipindi kinachorejewa," amesema Dkt. Kiruswa.

Aidha, Dkt. Kiruswa ameongeza kuwa, Madini mengine yanayopatikana katika Wilaya hiyo ni madini ujenzi aina ya mchanga , chuma, Shaba, makaa ya mawe na chokaa ambayo kwa sehemu yamechangia katika ujenzi wa barabara zinazounganisha Wilaya hiyo na maeneo mengine nchini.

Mkoa wa Kigoma umeunganishwa na wilaya nane , kakonko, kasulu, kibondo , uvinza, Buhigwe, Kusulu vijijini , Kigoma mjini na kigoma vijijini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news