Mafao ya wastaafu kulipwa ndani ya siku 60

DODOMA-Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi amelihakikishia Bunge kuwa mpango wa Serikali uliopo kwa sasa ni kulipa wastaafu mafao yao ndani ya siku 60 kwa mujibu wa sheria.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete akiteta jambo na Naibu Waziri wa ofisi hiyo, Mhe. Patrobas Katambi, Bungeni leo Agosti 29, 2024 jijini Dodoma.

Mhe. Katambi ameyasema hayo Agosti 29, 2024 bungeni alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Shaurimoyo, Ali Juma Mohamed ambaye amehoji Serikali ina mpango gani wa kuharakisha malipo ya wastaafu nchini.

Akijibu swali hilo, Mhe. Katambi amesema mpango huo umetokana na kuboreshwa kwa mifumo ya ulipaji wa mafao.
“Kwa Mfuko wa PSSSF kwa mwaka wa fedha 2023/24, wastaafu walioomba kustaafu ni 8,957, kati yao 5,016 wote tayari wamelipwa mafao yao ndani ya siku 60, wale wengine 3,941 ambao wanachangamoto ya waajiri kutopeleka michango na upungufu wa nyaraka yameendelea kushughulikiwa na yanapofikia mwisho ndani ya wiki mbili anakuwa amelipwa,”amesema.

Naibu Waziri Katambi amesema kwa Mfuko wa NSSF kulikuwa na maombi ya wastaafu 3,344 kati yao 3,325 tayari wamelipwa mafao yao ndani ya siku 60 na wamebaki 16 ambao wameendelea kushughulikia changamoto ya waajiri kuwacheleweshea michango na kesi zao zipo mahakamani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news