Kamishna Msaidizi wa Idara ya Usimamizi wa Madeni, Wizara ya Fedha, Bw. Omary Khama, akizungumza jambo siku ya pili ya Mafunzo kwa Taasisi za Serikali, kuhusu matakwa ya Sheria ya Mikopo, Dhamana na Misaada, Sura 134 na Miongozo mbalimbali kwenye ufadhili wa miradi ya maendeleo, katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania, jijini Dar es Salaam.
Mchumi Mwandamizi kutoka Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Bi. Tunukiwa Kavana, akizungumza kuhusu namna walivyopokea mafunzo yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha kuhusu elimu ya matakwa ya Sheria ya Mikopo, Dhamana na Misaada, Sura 134 na Miongozo mbalimbali kwenye ufadhili wa miradi ya maendeleo, kwa siku ya pili, iliyofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania, jijini Dar es Salaam, ambapo kwa siku ya pili wamejifunza namna ya kuandaa miradi kwa njia ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP).
Mkuu wa Kitengo cha Uchambuzi wa Miradi Kituo cha Ubia kati ya Sekta Binafsi na Sekta ya umma (PPP Center), Bw. Alfred Misana, akieleza namna ya kuandaa miradi kwa njia ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP), kwa washiriki wa mafunzo yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha kwa Taasisi za Serikali yaliyolenga kuwapa elimu ya matakwa ya Sheria ya Mikopo, Dhamana na Misaada, Sura 134 na Miongozo mbalimbali kwenye ufadhili wa miradi ya maendeleo, iliyofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania, jijini Dar es Salaam.
Mchumi kutoka Idara ya Usimamizi wa Madeni Wizara ya Fedha, Bw. Juma Mbarouk, akizungumza jambo Siku ya Pili ya mafunzo yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha kwa Taasisi za Serikali kuhusu elimu ya matakwa ya Sheria ya Mikopo, Dhamana na Misaada, Sura 134 na Miongozo mbalimbali kwenye ufadhili wa miradi ya maendeleo, iliyofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania, jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Washiriki kutoka Taasisi za Serikali wakifuatilia mafunzo yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha kuhusu elimu ya matakwa ya Sheria ya Mikopo, Dhamana na Misaada, Sura 134 na Miongozo mbalimbali kwenye ufadhili wa miradi ya maendeleo, kwa siku ya pili, iliyofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania, jijini Dar es Salaam.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,Wizara ya Fedha).