Magazeti leo Agosti 10,2024

DODOMA-Jeshi la Polisi Tanzania limewakamata watuhumiwa wanne kati ya sita ambao walipanga na kutekeleza uhalifu wa kumbaka na kumlawiti msichana na kusambaza video yake mitandaoni ambapo imebainika tukio hilo lilifanyika Swaswa jijini Dodoma mwezi Mei, 2024.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Agosti 9,2024 na Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime.

“Watuhumiwa hao wamekamatwa Mkoani Dodoma na Mkoa wa Pwani ambao ni Clinton Honest Damas kwa jina maarufu Nyundo, Praygod Edwin Mushi, Amini Lord Lema na Nickson Idala Jakson.

“Uchunguzi unaendelea kukamilishwa sambamba na kuwasaka Watuhumiwa wawili ambao bado wamejificha ili wafikishwe Mahakamani, kwa hawa ambao bado wamejificha kama kuna yeyote anayefahamu wamejificha kwake atoe taarifa na asipofanya hivyo wakikamatwa wakiwa nyumbani au kwenye makazi yake atakamatwa na kufikishwa Mahakamani."













Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news