GEITA-Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Balozi Dkt.Emmanuel Nchimbi amemuagiza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mheshimiwa Daniel Sillo kuwaachia huru viongozi wote wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wanaoshikiliwa na polisi jijini Mbeya.

"Kwa kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani upo hapa, mambo ya sheria sio ya kutolea maelekezo Kiongozi wa chama cha siasa, lakini nitumie nafasi hii mwambie Waziri wako kwamba tunaomba muone uwezekano wale viongozi wa vyama vya siasa waachiliwe ili mtupe nafasi ya kuzungumza nao.
"Kwa sababu tunajenga Taifa moja tunapenda kuwa na Taifa tulivu kama kuna maeneo wamekosea wao au tumekosea sisi tukae tuzungumze tuijenge nchi yetu."
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo