DAR-Mfanyakazi wa Kampuni ya Mabasi ya Japanese katika Kituo cha Mabasi cha Kimataifa cha Magufuli (Mbezi Magufuli Bus Terminal) aitwaye Atukuzwe Nyato ametoweka nyumbani kwake katika mazingira ya kutatanisha tangu Jumapili ya Agosti 11, 2024 alipoaga kwenda kununua dawa na sasa familia yake inamtafuta na kuomba msaada kwa yeyote mwenye taarifa zake.






Aliaga nyumbani akiwa amevaa gauni la rangi ya njano na nyeusi ambapo ndugu zake wamesema alitoweka akiwa maeneo ya Kibanda cha Mkaa Mbezi huku marafiki, ndugu na wafanyakazi wenzake wa kampuni ya Mabasi ya Japanese wameendelea na jitihada za kumtafuta katika maeneo mbalimbali hadi sasa bila mafanikio.



Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo