DODOMA-Watuhumiwa wanne kati ya sita wanaokabiliwa na kesi ya kubaka na kulawiti ambao video yao ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii ikionesha wakifanya kitendo hicho, wamefikishwa mahakamani Agosti 19,2024.
Watuhumiwa hao waliofikishwa mahakamani ni MT. 140105 Clinton Honest Damas maarufu Nyundo, Amin Lord Lema,Nickson Idala Jackson na C.1693 Playgod Edwin Mushi.
Watuhumiwa hao wamefikishwa katika Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki, Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dodoma na kusomewa makosa mawili ambapo kosa la kwanza ni kubaka kwa kundi na kosa la pili ni kumuingilia kinyume cha maumbile binti huyo.
Renatus Mkude ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Taifa ya Mashtaka amesema, kesi hiyo itasikilizwa kwa siku tano kuanzia Agosti 19 hadi Agosti 23,2024.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo