Magazeti leo Agosti 25,2024

SHINYANGA-Mtoto mchanga wa kike aliyeibwa Agosti 20,2024 saa 12:00 jioni katika Kijiji cha Mbika katika Kituo cha Afya Ushetu wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga amepatikana akiwa hai.
Hayo yamebainishwa Agosti 24,2024 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Janeth Magomi ambapo amesema, mtoto huyo alizaliwa Agosti 17,2024 na aliendelea kuwepo kituo cha afya kwa uangalizi zaidi,lakini siku ya tukio baada ya Mama yake mzazi kutoka nje kufanya mazoezi ndipo mtuhumiwa alimuiba mtoto huyo.
Magomi amesema taarifa za tukio hilo ziliripotiwa kituo cha Polisi Nyamilangano Agosti 21,2024 na ufuatiliaji wa haraka ulifanyika na Agosti 22,2024 saa tatu usiku Polisi walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa aitwaye Hadija Juma (24) mkazi wa Kijiji cha Sengerema Wilaya ya Uyui Mkoa wa Tabora akiwa na mtoto huyo.
“Mtuhumiwa huyo baada ya kumhoji amekiri kuwa aliiba mtoto baada ya kuolewa mara mbili bila ya kufanikiwa kupata mtoto ambapo aliolewa Ushetu miaka miwili hakupata mtoto akaolewa Wilaya ya Uyui hakupata mtoto, hivyo aliamua kuiba mtoto,” alisema huku taratibu za kumfikisha mahakamani mtuhumiwa huyo zikiendelea.








Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news