Magazeti leo Agosti 27,2024

MOROGORO-Wananchi wa Kijiji cha Kidogobasi Kata ya Ruhembe Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro wamefunga huduma za kijamii za shule, zahanati na ofisi ya Kijiji kwa lengo la kuishinikiza Serikali kutatua mgogoro wa shamba kati ya watu 21 na Serikali ya kijiji hicho.
Wananchi wa kijiji hicho Agosti 26,2024 wakiongozwa na Mwenyekiti Rashid Mteleka wamesema, wanatambua athari za kufanya jambo hilo, lakini wamelazimika kufanya hivyo ili viongozi wa Serikali waweze kuingilia kati na ufumbuzi upatikane.

Pia,wamesema shamba hilo lina ukubwa wa hekari 108 na kwamba kati ya hizo hekari 78 ndio zenye mgogoro kati ya Serikali ya kijiji na wananchi hao 21 ambao hivi karibuni wanadaiwa kuharibu mazao katika shamba hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Shaka Hamdu Sahaka akiongea kwa njia ya simu na waandishi wa habari amesema,suala hilo ni la kisheria na tayari timu ya wataalamu wa sheria pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri Wilaya Kilosa wameanza kupitia nyaraka mbalimbali na watakapojiridhisha Serikali itatoa tamko kuhusu mgogoro huo wa muda mrefu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news