Magazeti leo Agosti 31,2024

DAR-Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu raia wa Marekani, Brandon Dashaurn Summerlin kutumikia kifungo cha miaka 30 gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya Mescaline zenye uzito wa gramu 56.04.
Aidha, Mahakama hiyo imeamuru kielelezo ambacho ni gramu 56.04 za dawa za kulevya aina ya Mescaline kiharibiwe kwa mujibu wa Sheria ya Dawa za Kulevya nchini.
Hukumu hiyo imetolewa Agosti 29,2024 na Hakimu Mkazi Mwandamizi wa mahakama hiyo, Fahamu Kibona ambaye amesema, mahakama imeridhika na ushahidi wa mashahidi tisa wa upande wa mashtaka waliofika mahakamani hapo kutoa ushahidi wao dhidi ya mshtakiwa na vielelezo saba vilivyotolewa katika kuthibitisha mashtaka.

Awali ilielezwa kuwa, Novemba 12, 2022 huko Posta ndani ya Wilaya ya Ilala mkoani Dar es Salaam,maafisa wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA) walimkamata mshtakiwa akiwa anachukua kifurushi chenye dawa hizo ambazo aliziagiza kutoka nchini Peru.

Kufuatia kukamatwa kwake, mshtakiwa Brandon alifikishwa mahakamani na kushtakiwa kwa kosa moja la kusafirisha dawa za kulevya aina ya Mescaline.

Hakimu Kibona amesema, upande wa mashtaka umeweza kuthibitisha pasipo kuacha shaka kuwa mtuhumiwa alitenda kosa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news