MANYARA-Wafugaji wanaoishi ndani ya eneo la Hifadhi ya Jamii ya Wanyamapori ya Burunge (Burunge WMA) wilayani Babati Mkoa Manyara na jirani na maeneo hayo, wamejengewa mazizi ya waya (boma hai) ili kuzuia wanyama wakali hasa simba na fisi kuvamia na kula mifugo nyakati za usiku.
Mazizi hayo yamejengwa na Taasisi ya Uhifadhi na Utalii ya Chem Chem, ambayo inafanya shughuli za uhifadhi na utalii katika eneo hilo, lilipo kati kati ya hifadhi ya Taifa ya Tarangire na Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara ikiwa ni sehemu ya mkakati wa taasisi hiyo, kupunguza migogoro baina ya wanyamapori na mifugo.
Akizungumza wakati wa kukabidhi mazizi hayo, Mkuu wa Wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara, Lazaro Twange amesema,mradi wa ujenzi mazizi hayo ni utekelezaji wa maagizo ya Serikali kupunguza migogoro baina ya wanyamapori na binadamu.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo