LONDON-Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Uingereza,Mheshimiwa Mbelwa Kairuki amesema kuanzia juzi kuna ujumbe mfupi wa video uliozunguka katika mitandao ya kijamii uliorekodiwa na raia wa Uingereza mwenye asili ya Tanzania,Martina Farrall, akielezea maisha yake kuwa hatarini huko anapoishi Ireland ya Kaskazini.
Kwa mujibu wa taarifa aliyoitoa Agosti 6,2024 Balozi Kairuki amesema kufuatia ujumbe huo, Ubalozi umewasilisha taarifa ya Martina kwa mamlaka za Uingereza na kuomba hatua za kufuatilia suala hilo zichukuliwe mapema iwezekanavyo ili kuhakikisha usalama wake sambamba na kufanyia kazi tuhuma alizotoa ili kubaini ukweli wake na hatua kuchukuliwa.
“Aidha, leo tarehe 6 Agosti 2024 Afisa Ubalozi wa Tanzania anakwenda Ireland ya Kaskazini katika Mji anapoishi Bi. Farrall ili kukutana na mamlaka zinazohusika kufuatilia suala hilo.”
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo