Magazeti leo Septemba 1,2024

KILIMANJARO-Mkuu wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro,Mheshimiwa Kasilda Mgeni amelazimika kufunga jengo lililokuwa likitumika kama nyumba ya ibada maarufu Kanisa la Nabii Elia Msangi, baada ya kupata taarifa za kanisa hilo kuendeshwa kinyume na taratibu za sheria ya nchi. Pia,kudaiwa kuwepo kwa vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia na vitendo vingine vya mmomonyoko wa maadili kanisani hapo.
Mheshimiwa Mgeni ametoa maagizo hayo wakati wa ziara yake akiwa ameambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya walipotembelea eneo lilipo kanisa hilo Kitongoji cha Ikongwe A Kata ya Msindo na kujiridhisha taarifa za kuwepo viashiria vya matukio yasiyofaa yanayodaiwa kufanyika kwenye nyumba hiyo inayotumika kama kanisa na kubaini hakuna usajili wowote

Amesema, miongoni mwa sababu za kufunga kanisa hilo ni kuendeshwa pasipokuwa na usajili hali ambayo imepelekea kutojulikana ni dhehebu gani la dini, lakini pia hata uongozi unaosimamia kanisa hilo haujulikani mahali popote kwa kuwa kanisa halipo kwenye orodha ya taasisi za kidini zilizosajiliwa nchini.







Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news