Majaliwa ashuhudia wanachama 24 wa CUF, ACT Wazalendo wakirejea CCM ndani ya saa 48

LINDI-Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Mbunge wa Ruangwa, Kassim Majaliwa ameshuhudia wanachama 24 wa vyama vya CUF na ACT-Wazalendo wakirejea CCM ndani ya siku mbili.
Mheshimiwa Majaliwa alishuhudia wanachama hao wakikabidhi kadi zao kwa Katibu wa CCM wa Wilaya ya Ruangwa, Bw. Abbas Mkwenda (Agosti 23 na 24, 2024) wakati akizungumza na wakazi wa vijiji vya Mtondo (Kata ya Nambilanje) na Namikulo (Kata ya Chunyu), wilayani Ruangwa, Lindi ambako alifanya ziara ya jimboni kwake.

Katika kijiji cha Mtondo, wanachama tisa wa CUF walirejesha kadi zao wakiongozwa na Mzee Bakari Abdallah Nanyambo ambaye alikuwa Mwenyekiti wa CUF Kata ya Nambilanje. Wengine ni Abdallah Ally Manjawila, Bakari Ally Nyanga, Bakari Abdallah Nampota, Mwanahawa Abdallah Komaje, Zaituni Omary Mitachi, Mwanahawa Rashid Chomwingo, Somoe Omary Mkupete na Amina Musa Pachela.

Katika kijiji cha Namikulo, wanachama watano wa ACT-Wazalendo walikabidhi kadi zao wakiongozwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa ACT Kata ya Chunyu, Bw. Rashid Ibrahim Nakotyo. Wengine kutoka chama hicho ni Jafari Ali Namkwacha, Maulid Juma Mbanda, Mwajibu Saidi Baluya na Sefu Salum Makukuta.

Wengine 10 waliohama kutoka CUF ni Juma Abdalla Ching’oma (Mwenyekiti wa Kata), Said A. Mnunguye, Mohamed Selemani Lipei, Zena Rajabu Kabanda, Mohamed Mhumbila, Ally Mohamed Maluva, Abdalla M. Mbandula, Mwanaidi Saidi Mpingo, Idi Abdalla Matwani na Said Juma Mkomole.

Akizungumza baada ya kupokewa, Mzee Bakari Abdallah Nanyambo alisema ana uzoefu wa miaka 31 kwenye mageuzi na kwa sehemu kubwa alikuwa meneja wa kampeni kwa hiyo yuko tayari kutumia uzoefu wake akiwa ndani ya CCM.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news