DODOMA-Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Philip Isdor Mpango ameitaka Wizara ya Madini kuhakisha inasimamia vyema uvunaji wa madini ya kimkakati ili nchi iweze kunufaika nayo.

"Mwenyezi Mungu ametujaalia rasilimali hii ya madini mkakati yenye mahitaji makubwa sana Duniani," amesema Dkt. Mpango.
Amesema Mkoa wa Dodoma umebarikiwa kuwa na madini mkakati kwa wingi na aina tofauti tofauti, na kueleza kuwa ni lazima rasilimali hiyo ikatafsirike katika maendeleo ya wananchi wa Dodoma na Tanzania kwa ujumla.
"Wizara ya Madini hakikisheni mnaweka mpango mzuri wa usimamizi wa rasilimali hii kwa manufaa ya Taifa na kwa manufaa ya vizazi vijavyo,” amesema Dkt. Mpango.

