Mashujaa FC yaichapa Dodoma Jiji bao 1-0

NA DIRAMAKINI

MASHUJAA FC ya Kigoma imeanza vema Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya kujikusanyia alama tatu za ushindi wa bao moja.
Ni kupitia mtanange uliopigwa Agosti 17,2024 katika dimba la Lake Tanganyika mkoani Kigoma kati ya Mashujaa FC na Dodoma Jiji.

Wenyeji hao walijipatia bao hilo la kwanza kwa msimu wa 2024/25 baada ya mlinda lango wa Dodoma Jiji, Daniel Mgore kujifunga.

Ushindi huu unaipandisha Mashujaa hadi kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya NBC 2024/2025 huku Dodoma Jiji ikishuka hadi nafasi ya mwisho kwenye msimamo.

Ligi hiyo itaendelea tena Agosti 18,2024 kwa michezo miwili mchezo wa mapema saa 8:00 mchana utazikutanisha KenGold dhidi ya Singida Black Stars kwenye uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya.

Aidha,mchezo wa pili saa 10:15 alasiri utazikutanisha Simba dhidi ya Tabora United kwenye Uwanja wa KMC uliopo Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es salaam.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news