Matumizi sahihi ya mbolea,teknolojia utavuna zaidi-Mheshimiwa Mwassa

KAGERA-Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Fatma Mwassa amewataka wakulima mkoani humo kuacha kilimo cha mazoea kwa kuanza kutumia teknolojia mbalimbali ikiwemo matumizi sahihi ya mbolea katika shughuli zao za kilimo ili kuongeza uzalishaji na kukuza uchumi.
Amesema yeye ni mkulima wa mpunga mkoani Morogoro na kwamba amelima hekari 12 na kuvuna gunia 400 za mpunga ambazo ni sawa na gunia 33 kwa ekari moja.

Wakati kipato kitokanacho na mavuno hayo endapo bei ya gunia itakuwa nzuri ni hadi milioni 40 na hivyo kuwasihi wana Kagera kuona wivu na kuona fursa wanayoipoteza kwa kutokutumia mbolea.
Mkuu wa Mkoa Mwassa ameyasema hayo leo Agosti 14, 2024 alipokuwa akizungumza na wakulima wa Mkoa wa Kagera wakati wa ufunguzi wa kampeni ya "Kilimo ni Mbolea" inayolenga kuelimisha umma kuhusu matumizi sahihi ya mbolea na kuhamasisha usajili wa wakulima kwenye mfumo wa ruzuku ya mbolea.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mhe. Fatma Mwassa akizungumza na wakulima (hawapo pichani) alipokuwa akizindua kampeni ya 'Kilimo ni Mbolea' iliyoandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) katika ukumbi wa K's Missenyi mkoani Kagera tarehe 14 Agosti, 2024.

Amewataka wakulima kujitokeza kujisajili kwenye mfumo ruzuku ya mbolea ili waweze kununua pembejeo hiyo kwa bei nafuu kwa kuwa Serikali imeweka imeweka ruzuku inayotolewa kwa wakulima kupitia mfumo huo.
Wakulima na Maafisa kilimo wa Halmashauri za Wilaya ya Missenyi wakifuatilia mada kutoka kwa wataalam wa mbolea wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Kilimo ni Mbolea iliyofanyika katika ukumbi wa K's Missenyi mkoani Kagera tarehe 14 Agosti, 2024.

Sambamba na uzinduzi wa kampeni hiyo, Mkuu wa Mkoa Mwassa amezindua shindano la usajili wa wakulima kwa wilaya zote za mkoa wa Kagera na kueleza Wilaya itakayoibuka mshindi kwa kusajili wakulima wengi ifikapo Desemba 2024 itazawadiwa.
Wakulima na Maafisa kilimo wa Halmashauri za Wilaya ya Missenyi wakifuatilia mada kutoka kwa wataalam wa mbolea wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Kilimo ni Mbolea iliyofanyika katika ukumbi wa K's Missenyi mkoani Kagera tarehe 14 Agosti, 2024.

Pamoja na hayo, amewataka maafisa ugani wa Kila Halmashauri kutumia vizuri vifaa vya kupima udongo vilivyotolewa na Serikali kupitia Wizara ya Kilimo ili kuwawezesha wakulima kutumia mbolea kuendana na uhitaji wa udongo wanaolima.
Mwenyekiti wa Bodi ya TFRA, Dkt. Anthony Dialo akizungumza na wakulima wa Misenyi wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuelimisha umma juu ya matumizi sahihi ya mbolea na kuwahamasisha kujisajili kwenye mfumo wa mbolea za ruzuku kupitia kampeni ya Kilimo ni Mbolea tarehe 14 Agosti, 2024.

Kwa upande mwingine, Mwenyekiti wa Bodi ya TFRA, Dkt. Anthony Diallo amesema, mkulima anayetumia mbolea anapata mara kumi zaidi ya yule asiyetumia mbolea kwa kuwa anaweza kulima eneo dogo na kuvuna zaidi tofauti na mkulima anayelima eneo kubwa bila kutumia mbolea maana anatumia nguvu kubwa kwa mavuno kidogo.
Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) Kanda ya Ziwa, Michael Sanga akitoa elimu ya matumizi sahihi ya mbolea kwa wakulima wa Missenyi ambapo Mkuu wa Mkoa wa Kagera Fatma Mwassa alizindua kampeni hiyo tarehe 14 Agosti, 2024.

Amesema, kwa mwaka huu mamlaka inajikita katika kuhamasisha matumizi ya mbolea kwenye zao la migomba na kahawa ili kuongeza tija ya uzalishaji kwenye mazao hayo ambayo ndio mazao makuu katika mkoa huu.
Mkuu wa Sehemu ya Mipango na Ufuatiliaji wa TFRA, Eliurd Mwaiteleke akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa TFRA, Joel Laurent wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Kilimo ni Mbolea iliyofanyika katika ukumbi wa K's Misenyi mkoani Kagera tarehe 14 Agosti, 2024.
Wakulima na Maafisa kilimo wa Halmashauri za Wilaya ya Missenyi wakifuatilia mada kutoka kwa wataalam wa mbolea wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Kilimo ni Mbolea iliyofanyika katika ukumbi wa K's Missenyi mkoani Kagera tarehe 14 Agosti, 2024.

Uzinduzi huo ulihudhuriwa na viongozi wa juu wa Mkoa wa Kagera, Wilaya, kata na vijiji, wakulima wa Wilaya ya Missenyi pamoja na kampuni za mbolea za Itracom na Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news