Maxi Mpia Nzengeli aifanya Ubaya Ubwela kuwa chungu kwa Simba, Yanga SC yawachapa bao 1-0

NA DIRAMAKINI

MAXI Mpia Nzengeli ameifanya kauli mbiu ya Simba SC ya Ubaya Ubwela kuwa chungu baada ya kuwachapa watani hao bao 1 ambalo lilidumu hadi dakika 90 katika Ngao ya Jamii.
Nzengeli ambaye ni mwajiriwa wa Young Africans Sports Club (Yanga SC) ameiwezesha klabu kuonesha ukubwa wa kauli mbiu yao kuwa Nyie Hamuogopi?.

Simba na Young Africans Sports Club wamechuana leo Agosti 8,2024 katika Dimba la Benjamin Mkapa lililopo Halmashauri ya Manispaa Temeke jijini Dar Es Salaam.

Mchezo ulianza kwa kasi huku timu zikishambuliana kwa zamu, lakini kulikosekana umakini wa kutumia nafasi chache zilizotengenezwa na Simba katika dakika 30 za mwanzo.

Maxi Nzengeli aliipatia Yanga bao la kwanza dakika ya 43 kwa shuti kali la mguu wa kushoto baada ya kupokea pasi ya Prince Dube.

Kipindi cha pili, Simba SC walirudi kwa kasi na kufanya mashambulizi mengi langoni mwa Yanga na kutengeneza nafasi, lakini hawakuweza kuzitumia.

Pamoja na mashambulizi ya pande zote lakini hata hivyo hakuna kilichoweza kubadili matokeo.

Matokeo hayo yanawafanya Simba kukutana na Coastal Union katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu utakaopigwa Jumapili Uwanja wa Benjamin Mkapa saa tisa alasiri. Wakati  huo huo, Young Africans Sports Club itachuana na Azam FC katika fainali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news