Mheshimiwa Chumi ateta na Waziri Tsuji jijini Tokyo

TOKYO-Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Cosato Chumi (Mb) amekutana na kuzungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan Mhe. Kyoto Tsuji ofisini kwake jijini Tokyo.
Viongozi hao wamekubaliana kuendelea kushirikiana ili kuimarisha uhusiano na ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Japan kwa manufaa ya pande mbili
Akizungumza katika kikao hicho Mhe. Chumi aliishukuru Serikali ya Japan kwa kuendelea kuchangia maendeleo ya Tanzania katika sekta mbalimbali ikiwemo miundombinu, uwekezaji, elimu na afya.

Amesema Tanzania imejipanga kuhakikisha inaongeza kiwango cha biashara na uwekezaji kati yake na Japan na hivyo kuchochea ukuaji wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa manufaa ya pande zote mbili.
Naye, Mhe. Tsuji ameelezea utayari wa Japan kuendelea kushirikiana na Tanzania na kuimarisha uhusiano uliopo kwa manufaa ya nchi hizo.

Amesema, Japan itaendelea kushirikiana na Tanzania na kuongeza biashara na bara la Afrika ili kuhakikisha maendeleo ya kweli yanapatikana.Mhe. Chumia yuko nchini Japan kuhudhuria Mkutano wa Tisa wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu Maendeleo ya Afrika (TICAD) ngazi ya Mawaziri utakaofanyika jijini Tokyo tarehe 24-25 Agosti 2024.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news