Mheshimiwa Haroun azindua Light Upon Light

ZANZIBAR-Ujio wa Mufti Ismail Meky kutoka Nchini Zambia kutasaidia kuitangaza Zanzibar kiutalii wa kiislamu Duniani.

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Katiba,Sheria, Utumishi na Utawala Bora, Haruon Ali Suleiman ameyasema hayo leo wakati wa Uzinduzi wa Tamasha la Light Upon Light katika hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora,Haroun Ali Suleiman (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali katika hafla ya Uzinduzi wa Light Upon Light kuhusiana na Tamasha litakalofanyika kuanzia Oktoba 12 hadi 13,mwaka huu katika Uwanja wa Amani Complex ambapo masheikh kutoka nchi mbalimbali wanatarajiwa kushiriki akiwemo Mufti Menky kutoka Zimbabwe,hafla iliyofanyika Hoteli Verde Maruhubi Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora, Haroun Ali Suleiman akitoa hotuba ya Uzinduzi wa Light Upon Light.
Naibu Mufti Mkuu Sheikh Mahmoud Mussa Wadi akitoa hotuba ya Makaribisho kwa mgeni rasmi katika hafla ya Uzinduzi wa Light Upon Light.
Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mudrik Ramadhan Soraga akizungumza katika hafla ya Uzinduzi wa Light Upon Light.

Amesema, Mufti Meky ni Kiongozi maarufu duniani wa kiislamu ambaye anakubalika mwenendo vyema katika kutoa hamasa pamoja na kuhubiri amani na utulivu.

Sambamba na kutoa miongozo mbalimbali kwa umma wa kiislamu,hivyo ujio wake huo ni kuifungua Zanzibar katika kuleta mustakabali mwema wa kuitangaza kiutalii wa kiislamu.

“Zipo nchi kadhaa duniani zinafanya utalii wa kiislamu hii ni njia moja wapo ya kuwasili kiongozi huyu kwa lengo la kuitangaza Zanzibar kiiutalii wa kiislamu,"amesema Waziri Haruon.

Aidha, amesema Zanzibar ni chimbuko la historia za mashekh na Maulamaa Afrika Mashariki katika sehemu za kiislamu hivyo upowezekano mkubwa wakupokea walii wa ainahiyo inayo kubalika.

Naye Katibu Mtendaji Ofisi ya Mufti Mkuu Zanzibar, Shekh Khalid Ali Mfaume amesema Utalii wa kiislamu niwa kipekee ambao ofisiimeuridhia nakutoa ushirikiano kufanikisha Tamasha hilo.
Meneja Uhusiano kutoka PBZ, Fatma Aboud Talib akizungumza katika hafla ya Uzinduzi wa Light Upon Light.
Mwenyekiti wa Light Upon Light (NURU ALA NUR), Sheikh Nadir Mahfoudh akitoa taarifa maalum katika hafla ya Uzinduzi wa Light Upon Light.
Katibu wa Light Upon Light (NURU AL NUR) akitoa salamu za viongozi katika hafla ya Uzinduzi wa Light Upon Light.
Katibu Mtendaji Ofisi ya Mufti Mkuu Zanzibar, Sheikh Khalid Ali Mfaume akitoa salamu za Ofisi ya Mufti katika hafla ya Uzinduzi wa Light Upon Light.
Mwenyekiti wa Light Upon Light(NURU ALA NUR)Sheikh Nadir Mahfoudh akitoa taarifa maalum katika hafla ya Uzinduzi wa Light Upon Light.

Mapema Mwenyekiti wa Tamasha hilo,Sheikh Nadir Mahfoudh kutoka Annuor Cheretable alisema kuwa mpaka sasa zaidi ya nchi 12 duniani zimethibitisha kuwepo katika tamasha hilo ambalo mashekhe wakubwa watakuwemo katika kuleta umoja na mshikamano.

Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika Oktoba 12,mwaka huu katika uwanja wa Amani Complex Zanzibar likidhaminiwa na wafadhili mbali mbali wakiwemo PBZ Islamic,PDB,AMANA BANK,CRDB BANK.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news