Mheshimiwa Kapinga aeleza juhudi za Serikali kusambaza vituo vya CNG nchini

DODOMA-Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga amesema, kwa mwaka wa fedha 2024/2025 Serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania ( TPDC) inajenga vituo vya kujazia gesi kwenye magari (CNG) mkoani Dar es Salaam (viwili) na mkoani Pwani (kimoja).

Aidha,TPDC inaendelea na ununuzi wa vituo vidogo vya kujaza CNG kwenye magari vinavyohamishika ambavyo vitasimikwa katika mikoa ya Dar es Salaam (vitatu), Morogoro (kimoja) na Dodoma (viwili).
Mheshimiwa Judith Kapinga amesema hayo leo Agosti 27, 2024 bungeni jijini Dodoma wakati wa kipindi cha Maswali na Majibu.

Amesema, kwa sasa kuna vituo vitano vya kujazia gesi kwenye magari katika mikoa ya Dar es Salaam (Ubungo Maziwa, Tazara na Uwanja wa Ndege), Pwani (Mkuranga) na Mtwara (Dangote).

Kuhusu mpango wa magari ya Serikali kutumia mfumo wa CNG amesema kuwa tayari Mtaalam Mshauri ameshapatikana lengo likiwa ni kuhakikisha kwamba suala hilo linafanyika kwa ufanisi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news