Mheshimiwa Katambi azindua Kongamano la Vijana jijini Dodoma

DODOMA-Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,Mhe. Patrobas Katambi leo Agosti 10, 2024 amezindua Kongamano la vijana jijini Dodoma ikiwa ni kuelekea Siku ya Vijana Kimataifa Agosti 12, 2024.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,Mhe. Patrobas Katambi akihutubia vijana zaidi ya 3,000 kutoka maeneo mbalimbali nchini katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma leo Agosti 10,2024.

Kongamano hilo ambalo linaratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na kushirikiana na Wadau wa Maendeleo ya Vijana linalofanyika kwa siku mbili katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete ambapo takribani vijana 3,000 wamehudhuria.

Mhe. Katambi amesema asilimia 55.6 ya nguvu kazi ya taifa ni vijana na ndiyo kundi kubwa ambalo linategemewa sana katika kukuza uchumi na kuleta maendeleo na ustawi katika taifa.
Sehemu ya vijana wanaoshiriki Kongamano la Vijana jijini Dodoma leo Agosti 10,2024 ikiwa ni kuelekea Siku ya Vijana Kimataifa Agosti 12, 2024.

Aidha, amebainisha mikakati ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan namna ambayo imeendelea kukabiliana na changamoto ya ajira kwa vijana ikiwemo kusimamia na kuratibu programu za kukuza Ujuzi ili kuwezesha nguvu kazi kumudu ushindani katika soko la ajira.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,Mhe. Patrobas Katambi akihutubia vijana zaidi ya 3,000 kutoka maeneo mbalimbali nchini katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma leo Agosti 10,2024.

Vile vile, Mhe. Katambi amesema Serikali imeendelea kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo vijana katika masuala ya ujasiriamali, uanzishaji wa miradi ya kiuchumi, urasimishaji, uendeshaji wa biashara pamoja na uongozi ili kuendesha shughuli zao kwa weledi.

Sambamba na hayo, amesema Serikali inaendelea kuwawesha vijana kupata maeneo ya kufanyia shughuli za uzalishaji mali kwa kuhamasisha halmashauri zote nchini kutenga maeneo kwa ajili ya kufanyia shughuli za uzalishaji mali.
Sehemu ya vijana wanaoshiriki Kongamano la Vijana jijini Dodoma leo Agosti 10,2024 ikiwa ni kuelekea Siku ya Vijana Kimataifa Agosti 12, 2024.

Awali akizungumza Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu amehamasisha vijana kutumia vizuri kongamano hilo kujadili masuala mbalimbali yatakayokuza na kuimarisha ustawi wao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news