Mheshimiwa Kilangi atembelea banda la BoT maonesho ya Nanenane Zanzibar

ZANZIBAR-Katibu Mkuu, Wizara ya Maji, Nishati na Madini Zanzibar, Mhe. Joseph Kilangi, ametembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo - Nane Nane yanayoendelea visiwani Zanzibar katika viwanja vya Kizimbani-Dole, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Katibu Mkuu, Wizara ya Maji, Nishati na Madini Zanzibar, Mhe. Joseph Kilangi (wa saba kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa wa Benki Kuu baada ya kutembelea banda lao katika Maonesho ya Nanenane Zanzibar leo Agosti 10,2024.
Wakati wa ziara hiyo, Mhe. Kilangi alipata fursa ya kujifunza kuhusu majukumu mbalimbali yanayotekelezwa na Benki Kuu ya Tanzania.
Maonesho hayo ya saba tangu kuanza kufanyika visiwani Zanzibar, yanabebwa na kauli mbiu "Kilimo ni utajiri, kila mtu atalima,” na yanaendelea kufanyika hadi tarehe 14 Agosti, 2024.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news