Mheshimiwa Rukia Omar Mapuri awatembelea wasiojiweza jimboni

ZANZIBAR-Mwakilishi wa Jimbo la Amani, Mhe. Rukia Omar Mapuri amewaomba viongozi, wanachama na wananchi wa jimbo hilo kuendelea na utaratibu wa kuwatembea wagonjwa na wasiojiweza katika maeneo yao.
Ameyasema hayo wakati alipofanya ziara ya kuangalia viongozi wastaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambao ni wagonjwa na wasiojiweza katika Jimbo la Amani Wilaya ya Mjini.

Amesema, lengo la kufanya ziara hiyo ni kujua hali zao na kuwafariji ili wasijihisi wametengwa na jamii.

‘’Wenzetu hawa walipokuwa wazima walifanya mambo mengi mazuri,lakini kwa saa hizi hawezi tena hivyo ni wajibu wetu tuwe nao bega kwa bega viongozi wetu hawa,”alisema Mhe. Mapuri.

Aidha, amewataka kujenga ukaribu na upendo kwa viongozi hao ili waweze kujifunza njia mbalimbali walizozitumia wakati wa uongozi wao katika Chama, Jumuiya na Taifa kwa ujumla sambamba na kufahamu kuwa kila mtu ni mgonjwa mtarajiwa.

“Kama tunavyojuwa sisi sote ni wagonjwa watarajiwa,kwahiyo ni jambo zuri tukiwa na kawaida ya kuangaliana mara kwa mara na baadhi yao kama tunavyowaona tumefanya nao kazi pamoja kwa muda mrefu lakini leo wamepata changamoto ya kiafya,” alibainisha Mwakilishi huyo.

Nao baadhi ya wagonjwa waliotembelewa na Mwakilishi huyo wameomba, ziara hizo kufanyika mara kwa mara kwani zinawafariji na kuwapa moyo.

Hata hivyo, wamesema wanakabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwemo maradhi na baadhi yao kukosa matunzo stahili kwa familia.

Jumla ya watu 21 wametembelewa na Mwakilishi wa Jimbo la Amani Mhe. Rukia Omari Mapuri na kukabidhiwa vitu mbalimbali na fedha taslim.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news