MWANZA-Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Magdalena Rwebangira leo Agosti 14, 2024 ametembelea mafunzo ya Waandishi Wasaidizi ngazi ya Kata katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi na Kwimba mkoani Mwanza na kushudia watendaji hao wakiendelea na mafunzo.

Akiwa wilayani Misungwi, Mhe. Magdalena alishuhudia washiriki wakila kiapo cha kujitoa uanachama na kile cha kutunza siri.
Viapo hivyo vilifanyika mbele ya Hakimu wa Wilaya ya Misungwi, Mhe. Esther Anorld Marick.
Maafisa waandikishaji wasaidizi Ngazi ya Kata kutoka Kata zote za mkoa wa Mwanza wameanza mafunzo leo ambapo Agosti 21 wanaanza uboreshaji wa Daftari hadi Agosti 27, 2024.