Mheshimiwa Sangu ahimiza mafunzo ya uongozi kwa bodi mbalimbali

DAR- Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deus Sangu ameitaka Taasisi ya Uongozi kuweka kipaumbele kwenye mafunzo yanayohusisha wajumbe wa bodi mbalimbali za Mashirika ya Umma ili kujenga uelewa mpana wa masuala ya kiuongozi ili wanapofanya uamuzi wowote wazingatie maslahi mapana ya Taifa.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais UTUMISHI na Utawala Bora Mhe. Deus Sangu (Kulia) akiwa na Katibu Mkuu IKULU,Bw. Majula Mahendeka wakati alipokuwa akipata ufafanuzi wa jambo kutoka kwa Viongozi wa Taasisi ya Uongozi (hawapo pichani) wakati wa kikao chake cha kujifunza namna taasisi hiyo inavyofanyakazi kilichofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 16 Agosti, 2024.

Mhe. Sangu ametoa rai hiyo leo tarehe 16 Agosti, 2024 jijini Dar es salaam wakati alipofanya ziara ya kujifunza namna taasisi hiyo inavyofanya kazi na kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais UTUMISHI na Utawala Bora Mhe. Deus Sangu akizungumza na Viongozi wa Taasisi ya Uongozi (hawapo pichani) wakati wa kikao chake cha kujifunza namna taasisi hiyo inavyofanyakazi kilichofanyika Jijini Dar es Salaam tarehe 16 Agosti, 2024.

“Nimefarijika sana kusikia kuwa Taasisi ya Uongozi inatoa mafunzo mahususi ya kuwajengea uwezo wa kiutendaji viongozi mbalimbali ndani na nje ya Tanzania ikiwa pia ni sehemu ya utekelezaji wa jitihada za kuimarisha utawala bora.”
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais UTUMISHI na Utawala Bora Mhe. Deus Sangu akizungumza na Viongozi wa Taasisi ya Uongozi wakati wa kikao chake cha kujifunza namna taasisi hiyo inavyofanyakazi kilichofanyika Jijini Dar es Salaam tarehe 16 Agosti, 2024. Kushoto ni Katibu Mkuu IKULU Bw. Majula Mahendeka na Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Bw. Kadari Singo.

Ameongeza kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anafanya jitihada za kujenga nchi yetu katika nyanja mbalimbali, hivyo hatuna budi kumuunga mkono kwa kufanya mafunzo ambayo yanaweza kuwafanya viongozi mbalimbali kuwa wazalendo na wenye kiu ya kuona taifa linapata maendeleo.

Vile vile, amesisitiza watumishi wa Taasisi hiyo kuendelea na mshikamano katika kutekeleza majukumu yao kwa kuwa jukumu la kutoa mafunzo kwa Viongozi ni kubwa na linahitaji mshikamano.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais UTUMISHI na Utawala Bora Mhe. Deus Sangu akipata ufafanuzi wa jambo kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Bw. Kadari Singo wakati wa kikao chake cha kujifunza namna taasisi hiyo inavyofanyakazi kilichofanyika Jijini Dar es Salaam tarehe 16 Agosti, 2024.

Mhe. Sangu amefanya ziara katika Taasisi ya Uongozi kwa kwa lengo la kujifunza kuhusu majukumu ya Taasisi hiyo ambayo ipo chini ya Ofisi anayoiongoza.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news