DODOMA-Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Adolf Mkenda, Naibu Waziri Mhe. Omari Kipanga, Katibu Mkuu Prof. Carolyne Nombo na Naibu Katibu Dkt. Franklin Rwezamula wamekutana na Menejimenti ya Wizara, Viongozi wa Taasisi na Makamu wakuu wa Vyuo Vikuu kujadili utekelezaji wa vipaumbele pamoja na utekelezaji wa Sera na Mitaala mpya.


"Kwa kweli kuna umuhimu wa kuwa na mifumo inayosomana na kuzungumza pamoja hii itatuwezesha kupata takwimu sahihi za wanafunzi ili tujue walipo wanafunzi hata kama watakwenda kwenye mfumo wa Cambridge," amesema Waziri.
Aidha, Prof. Mkenda amesema ni muhimu kwa Vyuo Vikuu vinavyojenga kampasi mpya katika mikoa mbalimbali kuwa na programu za kutoa shahada za amali badala ya kutoa taaluma ambazo tayari zipo katika vyuo hivyo.