Miradi ya nishati itanufaisha wananchi wanaoizunguka-Kapinga

DODOMA-Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga amesema wananchi wanaoishi katika maeneo ambayo yana miradi mikubwa ya nishati watanufaika na miradi hiyo kupitia upatikanaji wa huduma mbalimbali.
Mhe. Kapinga amesema hayo Agosti 30, 2024 bungeni jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mhe. Ally Kasinge Mbunge wa Kilwa Kusini ambaye alitaka kufahamu mkakati wa Serikali katika kuhakikisha Kisiwa cha Songosongo mkoani Lindi ambako kuna visima vya Gesi Asilia na mitambo ya kuchakata gesi kinapata umeme wa uhakika.

"Mhe. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko alishatoa maelekezo kuhakikisha wananchi hawa sio tu wanapata umeme wa uhakika bali na huduma nyingine za kijamii ziweze kuimarishwa,"amesema Mhe. Kapinga

Amelihakikishia Bunge kuwa, tayari Serikali imeanza kulifanyia kazi agizo hilo kwa kuhakikisha wananchi wa Songosongo wanapata umeme wa uhakika na huduma nyingine za kijamii ambazo zinaendana na miradi iliyopo katika maeneo yao.

Akizungumzia upelekaji umeme wa gridi kwenye maeneo ya Visiwa, Mhe. Kapinga amesema Tanzania ina visiwa takriban 120 na Serikali imeanza kufanya tathmini ya kufikisha umeme wa gridi katika maeneo hayo.

Ameongeza kuwa, kwa sasa visiwa hivyo vinatumia umeme wa jua ambapo Serika imeweka ruzuku ya asilimia 50 hadi 55 ili wananchi wapate umeme wa uhakika kwa muda wote.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news