Mjasiriamali hatiani kwa kutumia nyaraka za uongo kujipatia mkopo SIDO

KAGERA-Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Kagera siku ya Agosti 26, 2024 imetoa hukumu dhidi ya mjasiriamali,Innocent Rwekaza na mwenzake, Bw. Jesper Josephat Balozi ambaye ni Karani wa Kampuni ya Kahawa TANICA PLC.
Mahakama hiyo imemtia hatiani Bw. Innocent Banyeza kwa makosa matatu ya kuwasilisha nyaraka za uongo na kujipatia mkopo kwa njia ya udanganyifu kutoka SIDO.

Ni kinyume na Kifungu cha 302 na 342 katika Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2022.

Hukumu hiyo dhidi ya Bw. Banyeza imetolewa katika Kesi ya Jinai Na. 38/2023 mbele ya Mhe. Wilson Yona SRM Hakimu Mkazi Mwandamizi - Mahakama ya Hakimu Mkazi Kagera.

Shauri hili limeendeshwa na mwendesha mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU),Bw. William Fussi.

Mshtakiwa wa kwanza amepewa adhabu ya kulipa faini ya shilingi 50,000 au kwenda jela mwaka mmoja kwa kila kosa la kutumia nyaraka za uongo.

Sambamba na kupewa adhabu ya kifungo cha nje miezi sita kwa kosa la kujipatia mkopo kwa njia ya udanganyifu.

Vilevile,ameamriwa na mahakama kurejesha kiasi cha sh. 2,500,000 alichokipata SIDO kwa udanganyifu.

Mshtakiwa wa pili yeye ameachiwa huru kwa kuwa taarifa ya kitaalamu ya maandishi haikuweka bayana ni nani aliyeghushi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news