Mtendaji wa Kata afikishwa mahakamani kwa kosa la ubadhirifu na ufujaji

LINDI (Agosti Mosi, 2024)- Katika Mahakama ya Wilaya Ruangwa imefunguliwa kesi ya Uhujumu Uchumi Namba 21635/2024, ya Jamhuri dhidi ya Mohamedi Selemani Mamba,aliyekuwa Mtendaji wa Kata ya Makanjiro wilayani Ruangwa.
Mshitakiwa anakabiliwa na kosa moja kwa mujibu wa hati ya mashitaka ambalo ni ubadhirifu na ufujaji kinyume na Kifungu cha 28(1) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329, Marejeo ya mwaka 2022.

Kifungu ambacho kinasomwa pamoja na Aya ya 21 ya Jedwali la kwanza pamoja na kifungu cha 57(1) na 60(2) cha Sheria ya Uhujumu Uchumi Sura ya 200 Marejeo ya mwaka 2022.

Mshtakiwa akiwa Mtendaji wa Kata ya Makanjiro kwa makusudi alibadilisha na kutumia kwa matumizi yake binafsi shilingi za 1,723,000 fedha ambayo ilitengwa kwa ajili ya kutengeneza madawati ya Shule ya Sekondari Makanjiro mwaka 2018.

Mshitakiwa amekamilisha masharti ya dhamana na kesi hiyo itatajwa mahakamani Agosti 20,2024.

Kesi hii inaendeshwa na wakili wa Serikali Yakubu Simba wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) Lindi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news