RUVUMA-Mahakama ya Wilaya ya Momba mkoani Ruvuma imemhukumu, Bw.Esau Andrew Hinjo aliyekuwa Askari wa SUMA JKT-Tunduma adhabu ya kwenda jela miaka mitatu au kulipa faini ya shilingi 500,000.
Ni kwa kosa la kuomba na kupokea hongo Kinyume na Kifungu cha 15(1) (a) na 2 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura 329 Marejeo ya Mwaka 2022.
Hukumu dhidi ya Esau Andrew Hinjo imetolewa katika Kesi ya rushwa Na.23763/2024 leo Agosti 21, 2024 mbele ya Hakimu Mkazi,Mheshimiwa Claud Msenjelwa wa Mahakama ya Wilaya ya Momba.
Kesi hiyo imeendeshwa na Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU), Bi.Lilian Matara.
Ilielezwa kuwa,mshtakiwa alifikishwa mahakamani kwa shtaka la kupokea hongo kiasi cha sh.120,000 toka kwa Joseph Itera Chunche kama kishawishi cha yeye kutokamata nyavu haramu za kuvulia samaki. Mshtakiwa alikiri makosa yake na kulipa faini ya sh.500,000.
Tags
Habari
Mahakamani Leo
SUMAJKT
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)
TAKUKURU Tanzania