Mwanamuziki Mandojo auawa akidhaniwa mwizi Dodoma

DODOMA-Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Joseph Francis maarufu kwa jina la Mandojo amefariki duniani akiwa mkoani Dodoma.
Kwa mujibu wa TBC Digital,taarifa ya awali zilizotolewa na mwanamuziki Domokaya ambaye pia waliwahi kuimba pamoja na mwingine Black Rhino zinasema, Mandojo amefariki dunia akiwa njiani akipelekwa hospitalini baada ya kushambuliwa na kupigwa na watu waliodhani kuwa ni mwizi.

Wakati wa uhai wake Mandojo akiwa na Domokaya waliwahi kutamba na vibao kama
Nikupe Nini (2003), Dingi (2004) na Taswira (2005) ambayo walimshirikisha Inspekta Haroun.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news