Mwanangu nieleze hapa Shule ya Wasichana ya Sayansi Kigoma mna changamoto gani?

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Tamisemi, Mhe. Mohamed Mchengerwa akimsikiliza kwa ukaribu Katibu Mkuu wa Serikali ya Wanafunzi wa Shule ya Wasichana ya Sayansi Kigoma Varelia Masele ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha tano, shuleni hapo.
Waziri Mchengerwa ametoa fursa hiyo kama sehemu ya kusikiliza changamoto za wanafunzi baada ya kuwa amewasikiliza viongozi na walimu wa shule hiyo.

Katika ziara yake shuleni hapo Waziri Mchengerwa amefanya ukaguzi wa ujenzi wa majengo mbalimbali yanayoendelea kujengwa shuleni hapo katika kuhakikisha shule hiyo inakidhi viwango vilivyotolewa na serikali katika ujenzi wa shule za sayansi za wasichana nchi nzima.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news