Mweka Hazina hatiani kwa ubadhirifu fedha za mikopo ya kikundi Ilala

DAR-Agosti 22, 2024 Mahakama ya Wilaya Ilala mkoani Dar es Salaam ilimtia hatiani mshtakiwa Sefania Adam Mwanja ambaye ni Mweka Hazina wa Kikundi cha Afya Jamii.
Bw. Mwanja alikabiliwa na makosa ya Kughushi, Uhujumu Uchumi na Utakatishaji wa fedha haramu katika shauri la Uhujumu Uchumi namba 9069/2024 lililofunguliwa Aprili 8, 2024 mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Mheshimiwa Aneth Nyenyema.

Shauri hilo lilihusisha jumla ya washtakiwa wanne wote wakiwa ni wanachama wa kikundi hicho, ambapo; Mshtakiwa Bw.Mwanja yeye alikiri kutenda makosa hayo kwa utaratibu wa maridhiano.

Aidha, amelipa shilingi milioni tano pamoja na kurejesha gari aina ya Toyota Premio yenye thamani ya shilingi milioni 17.

Gari hilo alinunua kwa fedha za mkopo wa shilingi milioni 100 na kulisajili kwa jina lake binafsi na hivyo ametakiwa kulirejesha kwenye umiliki wa kikundi.

Shauri hilo lilitokana na udanganyifu uliofanywa na washtakiwa hao wanne kwa pamoja, ambao walijipatia mkopo wa shilingi milioni 100 kutoka Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na kuzitumia fedha hizo kinyume na matumizi yaliyokusudiwa.

Aidha, shauri dhidi ya washtakiwa watatu waliosalia ambao ni: Erick Isack Gabriel, Sabina William Ndasi na Jacob Chacha Mwita litaendelea Septemba 18, 2024.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news