Mwenyekiti wa Bodi ya GST atoa maelekezo kuimarisha taasisi

DODOMA-Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) imeelekezwa kuendelea kuitangaza bidhaa inayoizalisha ya vyungu vya kuyeyushia sampuli za miamba na udongo wenye madini ya dhahabu (crucibles) ili kuongeza makusanyo ya ndani na kuongeza tija kwa taasisi.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Bodi ya GST Prof. Justinian Ikingura wakati akiongoza kikao cha 19 cha Bodi ya GST kilichofanyika Agosti 01, 2024 katika ukumbi wa Prof. Abdulkarim Mruma jijini Dodoma.
Aidha, Prof. Ikingura ameitaka Taasisi hiyo kuongeza jitihada za kujitangaza hasa katika huduma zitolewazo na maabara ya _geotechnical_ kwa wadau mbalimbali ili kuitumia GST katika utafiti na uchunguzi wa sampuli za miamba na udongo.
Aidha, Prof. Ikingura ameipongeza Menejimenti ya GST kwa kazi nzuri inayoendelea kuifanya na kuitaka taasisi hiyo kuandaa mpango wa kutoa elimu kwa wadau katika maeneo mbalimbali ikiwemo matumizi ya taarifa za jiosayansi katika utafutaji na uchimbaji wa madini; na ubora wa vyungu vya kuyeyushia sampuli za miamba na udongo wenye madini ya dhahabu kwa lengo kuongeza uelewa kwa watumiaji wa bidhaa hiyo.

Naye, Kaimu Mtendaji Mkuu ambaye pia ni Mkurugenzi wa Huduma za Maabara ya GST Notka Banteze amesema Menejimenti ya GST imepokea maelekezo ya Bodi hiyo na kuahidi kuyafanyia kazi maelekezo yote yaliyotolewa.
Pia, ameishukuru Bodi hiyo kwa ushauri na maelekezo waliyoyatoa ambapo ameahidi kutekeleza maelekezo yote yaliyotolewa na bodi hiyo.

Kikao hicho cha 19 cha Bodi ya GST kimelenga kujadili taarifa ya utekelezaji ya GST ya kipindi kinachoanzia Aprili hadi Julai 2024.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news