ARUSHA-Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Dennis Londo (Mb) ametembelea Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Masharki (EAC) Mhe. Veronica Nduva Ofisini kwake jijini Arusha.
Katika mazungumzo yao, Mhe. Londo alimuhakikishia Mhe. Nduva ushirikiano na kumuelezea kuwa Tanzania itashiriki katika masuala yote yanayohusu Jumuiya ya EAC kwa uzito unaostahiki.


