Naibu Waziri Sangu apata mapokezi makubwa Rukwa,amshukuru Rais Dkt.Samia

RUKWA-Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Mbunge wa Jimbo la Kwela, Mhe. Deus Sangu amewahakikishia wananchi kuwa atafanya kazi kwa weledi na uaminifu wa hali ya juu huku akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa heshima kubwa aliyowapa wananchi wa Jimbo la Kwela na Mkoa wote wa Rukwa kwa kumteua yeye kuwa Naibu Waziri wa ofisi yake.
Aidha, Mhe. Sangu amewashukuru wananchi wote wa Mkoa wa Rukwa kwa mapokezi makubwa waliyompa mara baada ya kuwasili Mkoani humo, ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo.

Mhe. Sangu ametoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti wakati akizungumza na Watumishi pamoja na wananchi katika Kata ya Kanda na Kaengesha kwenye mikutano ya hadhara iliyofanyika kwenye Vijiji vitano vya Jimbo la Kwela , Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa.
Amesema, Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amewaheshimisha wananchi wa Mkoa wa Rukwa kwa kumteua yeye ili aweze kumusaidia kuwahudumia Watanzania katika masuala ya utumishi na utawala bora.

"Naomba niwaahidi katika najukumu yangu haya mapya nitakuwa mnyenyekevu, mchapakazi, mweledi na mwaminifu katika kutekeleza majukumu yangu ya kumsaidia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene," amesema Mhe.Sangu.

Ameongeza kuwa, "Nawashukuru pia wananchi wa Kwela kwa kuniamini na kunituma Bungeni ili nikawesemee changamoto zinazowakabili hii imepelekea Rais Samia kuweza kuniona na kuniteua kushika wadhifa huu.
Katika hatua nyingine Mhe. Sangu ametumia fursa hiyo kumshukuru Mhe.Rais kwa kutekeleza miradi mingi ya maendeleo katika Jimbo la Kwela ikiwemo ujenzi wa zahanati, barabara, maji pamoja na umeme.

Mhe. Mhe.Sangu amewahakikishi wananchi hao kuwa, "Mambo mazuri zaidi yanakuja, Rais Samia amesema anataka kuiona Kwela yenye nuru kiuchumi," amesisitiza Mhe.Sangu.

Amesema, Mheshimiwa Rais anawapenda sana wananchi wake hususan wa Mkoa wa Rukwa ndio maana ameongeza bei ya mazao ya mahindi hadi Sh.700 kwa kilo moja ili kuhakikisha wananchi wa Kwela wananufaika kiuchumi kupitia kilimo chao.
Hata hivyo Mhe.Sangu ameowaonya wananchi wake wasithubutu kuuza mazao yote la sivyo kufikia Mwezi Januari mwakani watakumbwa na baa la njaa.
Kwa upande wake Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa, Mhandisi, Daudi Sebiga ametumia fursa hiyo kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumteua Mhe.Deus Sangu kwani Mchapakazi na Mwaminifu wa kiwango cha hali ya juu sana.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news