Naibu Waziri Sangu awaasa watumishi wa Serikali ya Ajira kuwajibika

NA VERONICA MWAFISI

NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu amewaasa Watumishi wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kuwajibika kwa viwango vikubwa katika kutekeleza majukumu yao ili kutimiza azma ya taasisi hiyo katika kutoa ajira kwa kutenda haki sawa kwa kila mwananchi.
Mhe. Sangu ameyasema hayo Agosti 22, 2024 wakati alifanya ziara yake ya kikazi iliyolenga kujifunza majukumu ya ofisi hiyo na kuhimiza uwajibikaji.
"Niwaase kuwajibika kwa viwango vikubwa katika kutekeleza majukumu yenu hasa kwa kutenda haki sawa kwa kila mwananchi atakayeomba ajira, zingatieni maadili ya taasisi hii kwa maslahi ya taifa," amesema Mhe. Sangu.
Aidha, Mhe. Sangu ameipongeza Menejimenti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuboresha na kurahisisha usaili kwa kutumia TEHAMA kwani haki inatendeka na inaijengea taasisi uaminifu mkubwa kutoka kwa wananchi.
Mhe. Sangu ameendelea na ratiba yake ya kutembelea taasisi mbalimbali zilizopo chini ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa lengo la kujifunza kuhusu majukumu ya taasisi hizo na kuhimiza uwajibikaji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news