Naibu Waziri Ummy apokea jedwali la uchambuzi wa Sheria Ndogo

DODOMA-Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu),Mheshimiwa Ummy Nderiananga amepokea Jendwali la Uchambuzi wa Sheria Ndogo za Mwaka 2024.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. Ummy Nderiananga akipokea jendwali la uchambuzi la Sheria Ndogo kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya sheria Ndogo Mhe. Ramadhan Suleimani Ramadhan.

Ni katika Mkutano wa Kumi na Tano, Kikao cha Sita cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambazo zimewasilishwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Sheria Ndogo, Mhe. Ramadhan Suleimani Ramadhan.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Sheria Ndogo, Mhe. Ramadhan Suleiman Ramadahan akiongoza kikao cha Kamati Ndogo ya Bunge ya Sheria Ndogo katika ukumbi wa Bunge jijini Dodoma.

Tukio hilo limefanyika leo Agosti 16,2024 katika Ukumbi wa Bunge jijini Dodoma.

Amesema, mafanikio ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) yanatokana na ushirikiano ambao umekuwa ukitolewa na Kamati ya Bunge ya Sheria ndogo.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Sheria Ndogo wakiwa katika Kikao wakati wa uwasilishaji wa Uchambuzi wa Jedwali kwa Naibu Waziri Ofisi ya waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga akizungumza wakati wa upokeaji wa Jendwali la Uchambuzi la Sheria Ndogo katika ukumbi wa Bunge jijini Dodoma.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Sheria Ndogo wakiwa katika Kikao wakati wa uwasilishaji wa Uchambuzi wa Jedwali kwa Naibu Waziri Ofisi ya waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga.

“Naomba niwahakikishie kamati, nimepokea jedwali hili na tutawasilisha kwa wizara zinazohusika ili zije zilete majibu, naomba tuendele kupata ushirikiano wakati wizara hizo zitakapokuja kuwasilisha,” amesema Naibu Waziri Ummy.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news