Naibu Waziri wa Uchukuzi atembelea banda la TMA maonesho ya Nanenane

DODOMA-Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kihenzile (MB) ametembelea banda la Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) katika kilele cha maonesho ya Nanenane 2024, Nzuguni, Dodoma.
TMA ni miongoni mwa mashirika na taasisi za umma ambazo zimeshiriki Maonesho ya Kilimo ya Kimataifa Nanenane 2024 yakiongozwa na kauli mbiu ya "Chagua Viongozi Bora wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi" ambapo yalifunguliwa Agosti 1,2024.
Kupitia maonesho hayo wananchi wamepata elimu kuhusu mamlaka hiyo ikiwemo sayansi ya hali ya hewa inavyofanya kazi na umuhimu wa mamlaka katika sekta ya kilimo nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news