Naibu Waziri wa Ujenzi amtaka Mkandarasi BRT3 kuboresha ujenzi




DAR-Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi, Godfrey Kasekenya amemtaka mkandarasi M/S SINOHYDRO COOPERATION LIMITED anayejenga miundombinu ya mfumo wa usafiri wa mabasi yaendayo haraka BRT 3, KM 23.3 kuanzia katikati ya jiji la Dar es salaam hadi Gongolamboto kuhakikisha ujenzi huo unajengwa kwa viwango vya kimataifa kutokana na umuhimu wa barabara hiyo.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Eng. Godfrey Kasekenya akisisitiza jambo kwa wataalam kutoka TANROADS wakati alipokagua maendeleo ya Ujenzi wa Barabara ya Mabasi yaendayo haraka BRT 3&4 Jijini Dar es Salaam leo.

Akikagua ujenzi wa barabara za mabasi yaendayo kwa haraka leo, Naibu Waziri Kasekenya amesema barabara hiyo ni lango la jiji la Dar es salaam na taifa kwa ujumla hivyo Serikali inategemea kuwa itakuwa barabara ya mfano kwa ubora na muonekano.
“TANROADS na Mkandarasi hakikisheni barabara hii inajengwa kwa viwango vya kimataifa vya ubora na muonekano kwani licha ya kuwa lango kuu la kuingia nchini pia ina historia ya kuitambulisha Tanzania kwa wageni,” amesema Eng. Kasekenya.

Aidha, amemtaka Mkandarasi kuweka mfumo mzuri wa kudhibiti maji ya mvua ambayo yamekuwa kero kwa miaka mingi katika barabara hiyo na kuhakikisha maji hayo yanaelekezwa kwenye mfumo mzuri ili kutoleta mafuriko kwenye makazi ya watu.
Muonekano wa moja ya vituo vya Mabasi yaendayo haraka BRT 3&4 Jijini Dar es Salaam, ambavyo ujenzi wake unaendelea.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Eng. Godfrey Kasekenya akisisitiza jambo kwa wataalam kutoka TANROADS wakati alipokagua maendeleo ya Ujenzi wa Barabara ya Mabasi yaendayo haraka BRT 3&4 Jijini Dar es Salaam leo.

Amezungumzia umuhimu wa mkandarasi kusimamia vizuri matumizi ya barabara wakati ujenzi ukiendelea ili watumiaji wa barabara wasipate adha na kusababisha msongamano na ajali zinazoweza kuepukika.

‘‘Barabara unganishi zinazounga BRT na barabara nyingine ziwe bora na salama wakati wote, wekeni alama za barabarani wakati huu wa matengenezo”, amesisitiza Naibu Waziri huyo.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Kasekenya amewataka wakandarasi watatu, wanaojenga BRT 4 kuongeza kasi ya ujenzi ili miradi hiyo ikamilike kwa wakati na kulifanya jiji la Dar es salaam kuondokana na msongamano wa magari.
Meneja Mradi wa BRT 4, Eng. Allen Natai (wa pili kulia) akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Eng. Godfrey Kasekenya wakati akikagua maendeleo ya Ujenzi wa Barabara ya Mabasi yaendayo haraka BRT 3&4 Jijini Dar es Salaam leo.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Eng. Godfrey Kasekenya akimsikiliza Eng. Mwanaisha Rajabu kutoka TANROADS wakati alipokagua maendeleo ya Ujenzi wa Barabara ya Mabasi yaendayo haraka BRT 3&4 Jijini Dar es Salaam leo.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Eng. Godfrey Kasekenya akisisitiza jambo kwa wataalam kutoka TANROADS wakati alipokagua maendeleo ya Ujenzi wa Barabara ya Mabasi yaendayo haraka BRT 3&4 Jijini Dar es Salaam leo.

Wakandarasi hao ni China Geo Engineering Corporation (CGC), anaeyejenga sehemu ya Maktaba ya taifa -Moroco-Mwenge –Ubungo km 13.5, M/S Shandong luquiao Group Co Ltd anayejenga barabara ya Mwenge hadi Tegeta Dawasa km 15.63 na Mkandarasi China Communication Construction Co. Ltd anaejenga karakana ya mabasi hayo Kivukoni, Mbuyuni na simu 2000.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news