New Amaan Stadium na Gombani Stadium kutumika Ligi Kuu Tanzania Bara

DAR-Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi ya Tanzania Bara (TPLB), Almas Kasongo amesema kuanzia msimu huu mpya wa mwaka 2024-2025 inaruhusiwa kwa timu za Ligi Kuu Tanzania Bara kutumia viwanja vya Zanzibar ikiwemo New Amaan Stadium Unguja na Gombani Stadium Pemba.
"Katikati ya msimu uliopita klabu ya Simba iliomba kuutumia uwanja wa New Amaan Complex, haikuwezekana kwa sababu kanuni zilikuwa haziruhusu, lakini hoja zao zilikuwa na mashiko.

"Tulikaa na Kamati Tendaji ya (TFF) tukaona haina haja ya kuzuia jambo hilo, hivyo tukafanya mabadiliko ya kanuni sasa wataruhusiwa kwa timu za Ligi kuu Tanzania Bara kutumia viwanja vya Zanzibar.

"Kanuni itaanza kutumika msimu huu 2024-2025," Almas Kasongo alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news