NGOs Pwani zatakiwa kutoa elimu kwa jamii kuelekea Uchaguzi

PWANI-Mkuu wa Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani, Simon Nickson ametoa wito kwa mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) yanayofanya kazi mkoani Pwani kutoa elimu kwa jamii ili kuwawezesha wananchi kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu na uchaguzi wa serikali za mitaa.
Nickson ametoa wito huo Agosti 28,2024 wakati akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Pwani katika mkutano wa Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NacoNGO) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani.
Ameeleza kuwa, wanawategemea katika kuhamasisha wananchi, kuongeza uelewa na kuwaelimisha kuhusu umuhimu wa kupiga kura.

Ameipongeza, NacoNGO kwa ushirikiano wake na serikali katika kutatua changamoto za wananchi, hususan suala la upatikanaji wa maji safi katika ngazi ya mkoa na kitaifa kwa ujumla.
Naye Mwakilishi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani, ambaye pia ni Katibu Tawala Msaidizi, Felix Ncalio amehimiza umuhimu wa ushirikiano kati ya mashirika yasiyo ya kiserikali na serikali, pamoja na ushirikiano kati ya mashirika yenyewe, ili kurahisisha utekelezaji wa mipango ya maendeleo.

Mwenyekiti wa NacoNGO, Jasper Makalla, amesisitiza umuhimu wa mashirika hayo kufanya kazi kwa kuzingatia maadili na kutoa ushirikiano katika kuwasilisha taarifa za kifedha ili kuwezesha mipango ya maendeleo.
Naye mjumbe wa baraza hilo kutoka Shirika la Mamas and Papas, ambaye pia ni Afisa Habari wa shirika hilo, Omary Kombe ametoa pendekezo la kuandaa kongamano la mkoa litakalowezesha mashirika kuonyesha shughuli mbalimbali wanazozifanya.
Pia, alishauri baraza kuanzisha mbio za marathoni zitakazowahusisha wadau mbalimbali kwa lengo la kuchangia na kushiriki ili kuongeza kipato cha mashirika hayo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news