NHC:Wananchi njooni mmiliki nyumba bora na za kisasa

NA DIRAMAKINI

SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) limetoa wito kwa wananchi kuendelea kuchangamkia fursa ya kumiliki nyumba bora na za kisasa kupitia miradi mbalimbali ya shirika inayotekelezwa nchini.
Hayo yamesemwa leo Agosti 4, 2024 katika Maonesho ya Kitaifa ya Kilimo Nanenane yanayoendelea viwanja vya Nzunguni jijini Dodoma na Abuu Ahmad Mwangu, Afisa Mauzo na Masoko wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Mkoa wa Dodoma.

Afisa huyo alikuwa anaelezea kuhusiana na miradi mbalimbali ya Shirika la Taifa la Nyumba (NHC) ambayo inatekelezwa katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

"Awali ya yote ninapenda kuwakaribisha kwenye banda letu la Shirika la Nyumba la Taifa ambalo lipo kwenye banda kuu la taasisi za Serikali hapa Nanenane ambapo Kitaifa ni hapa jijini Dodoma.

"Katika mkoa mwenyeji hapa Dodoma tuna mradi wa nyumba 1,000 ambao upo Chamwino na Iyumbu, lakini kwa sasa nyumba ambazo zipo ni katika eneo la Iyumbu ambako tunawakaribisha kwa ajili ya kuja kujipatia nyumba za ubora wa hali ya juu kabisa.
"Lakini, pia tuna miradi mingine ambayo ipo katika Jiji la Dar es Salaam, kwa kuenzi mchango mkubwa wa Rais wetu mpendwa Mama Samia Suluhu Hassan tuna mradi pale Kawe ambao tumeupa jina la Samia Housing Scheme, pale tuna nyumba ambazo zimejengwa na zipo katika hatua ya umaliziaji.

Lakini, pia tuna mradi ambao ulikuwa umesimama wa Seven Eleven (7|11), lakini sasa tunaendelea na ujenzi, mradi huu nafasi bado zipo, hivyo mnaweza kufika na kujipatia fursa ya kumiliki nyumba zenye ubora wa hali ya juu,"amefafanua Afisa Mauzo na Masoko huyo huku akiongeza kuwa,

"Lakini, pia tuna mradi wa Morocco wanauita Morocco Square, nyumba bado zipo na za kiwango cha ubora wa hali ya juu. Unakuja, unapata utaratibu wa kulipia na kununua nyumba unayoitaka kwa ajili ya umiliki.
"Hivyo, tunawakaribisha mtu yeyote ambaye yupo hapa Nanenane Dodoma au kwa yule ambaye yupo mkoa wowote, fika katika ofisi zetu ambapo utapata maelezo ya miradi hii iliyopo.

"Lakini, pia kwa hapa Dodoma kuna mradi ambao unakuja wa Medeli Phase 3 ambao utaanza ndani ya kipindi hiki cha mwaka huu wa fedha, kwa hiyo tunawakaribisha katika banda letu hapa Nanenane Dodoma mtapata maelezo ya kutosha."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news