Ni lazima kila mtumishi wa umma atumie Mfumo wa e-Utendaji Kazi-Mheshimiwa Sangu

DODOMA-Naibu Waziri, Ofisi ya Rais UTUMISHI na Utawala Bora Mhe. Deus Sangu ameyasema hayo tarehe 15 Agosti, 2024 wakati alipokuwa akifuatilia mawasilisho mbalimbali ya majukumu ya Idara ya Usimamizi wa Mikataba ya Utendaji Kazi Serikalini, Idara ya Usimamizi wa Maadili, Idara ya Usimamizi wa Huduma za TEHAMA Serikalini na Idara ya Mipango ikiwa ni sehemu ya kujifunza kuhusu majukumu ya Ofisi yake.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais UTUMISHI na Utawala Bora Mhe. Deus Sangu akizungumza na Idara ya Usimamizi wa Huduma za TEHAMA Serikalini wakati wa kikao cha kumpitisha katika majukumu ya Idara hiyo kilichofanyika Mtumba jijini Dodoma tarehe 15 Agosti, 2024.

Mhe. Sangu ameelekeza Idara ya Usimamizi wa Utendaji Kazi Serikalini kufuatilia watumishi wote wa umma mahali popote walipo ili kujua wanafanya nini na kwa maslahi ya nani.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais UTUMISHI na Utawala Bora Mhe. Deus Sangu akiptia nyaraka wakati wa kikao cha kumpitisha katika majukumu ya Idara mbalimbali kilichofanyika katika ukumbi mdogo wa ofisi hiyo tarehe 15 Agosti, 2024.

“Mfumo wa Kupima Utendaji Kazi kwa Watumishi wa Umma (e-Utendaji Kazi) ni matokeo ya maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na ni utekelezaji wa Sheria, Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Umma, hivyo ni lazima kila mtumishi wa umma kujiunga na kutumia mfumo huo na si hiari,” amesisitiza Mhe. Sangu.

Aidha, ametoa rai kwa idara hiyo kufanya utafiti na kubaini taasisi ambazo zinasuasua kutumia mfumo huo ili hatua za kinidhamu ziweze kuchukuliwa dhidi ya Maafisa Masuuli na watumishi wa Taasisi hizo.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais UTUMISHI na Utawala Bora Mhe. Deus Sangu akizungumza na watumishi wa Idara ya Usimamizi wa Mikataba ya Utendaji Kazi Serikalini wakati wa kikao cha kumpitisha katika majukumu ya Idara hiyo kilichofanyika katika ukumbi mdogo ulipo jengo la Utumishi jijini Dodoma tarehe 15 Agosti, 2024.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais UTUMISHI na Utawala Bora Mhe. Deus Sangu akimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Mipango Bw. Cosmas Ngangaji wakati wa kikao cha kumpitisha katika majukumu ya Idara hiyo kilichofanyika Mtumba jijini Dodoma tarehe 15 Agosti, 2024.

Kwa wakati mwingine ameelekeza Idara ya Usimamizi wa Maadili kutoa mafunzo ya maadili kwa watumishi wapya na walio kazini ili waweze kutambua na kujikumbusha misingi ya maadili katika utumishi wa umma.

“Kuna mambo yasiyofaa ambayo yako kinyume na maadili ya Utumishi wa Umma na yanaendelea katika ofisi za umma kutokana na watumishi hao kujisahau na kuzifanya ofisi hizo kuwa binafsi.

Hali kadhalika, ameipongeza Idara ya Huduma za TEHAMA Selikani kwa kubuni, kusanifu na kutengeneza mifumo ambayo inasimamia utendaji kazi katika utumishi wa umma.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais UTUMISHI na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu akimshukuru Mkurugenzi wa Idara ya Mipango Bw. Cosmas Ngangaji baada ya kikao cha kumpitisha katika majukumu ya Idara hiyo kilichofanyika Mtumba jijini Dodoma tarehe 15 Agosti, 2024.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais UTUMISHI na Utawala Bora Mhe. Deus Sangu akimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Maadili Bi. Leila Mavika wakati wa kikao cha kumpitisha katika majukumu ya Idara hiyo kilichofanyika Mtumba jijini Dodoma tarehe 15 Agosti, 2024.

Mhe. Sangu ameendelea na ratiba yake ya kujifunza kuhusu majukumu ya idara mbalimbali zilizopo katika ofisi yake yanayofanyika katika ukumbi mdogo wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mtumba jijini Dodoma.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news