GEITA-Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt.Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), amewaasa wananchi kuacha kugombana kwa sababu za siasa kwani kitendo hicho kinasababisha maafa, yatima, wajane na kukosekana kwa amani.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) akizungumza na waumini wa Kanisa la Waadventista mjini Katoro mkoani Geita kwenye kilele cha makambi.
Dkt.Nchemba ameyasema hayo kwenye kilele cha Makambi alipokuwa akizungumza na waumini wa Kanisa la Waadventista (Wasababato) Mjini Katoro mkoani Geita.






Dkt.Nchemba, amewaasa waumini hao kuepuka kujihusisha na siasa za fujo na vurugu kwasababu zinaleta madhara makubwa kwa familia moja moja na nchi kwa ujumla hivyo kuathiri uchumi, umoja na mshikamano wa Taifa.
Aidha, Dkt.Nchemba amewataka waumini hao kuendelea kumwombea Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ili aendeleze kudumisha maelewano, mshikamano na kusikilizana ambazo ndio zimekuwa falsafa zake tangu aingie madarakani.