Nishati safi ya kupikia yavutia wananchi Tamasha la Kizimkazi

ZANZIBAR-Wananchi waliofika katika Tamasha la Kizimkazi linaloendelea katika eneo la Kizimkazi Dimbani Mkoa wa Kusini Unguja wamevutiwa na teknolojia ya Nishati Safi ya Kupikia.Wakizungumza kwa nyakati tofauti Agosti 20. 2024 mara baada ya kutembelea Banda la REA na kushuhudia teknolojia za majiko ya Nishati Safi ya Kupikia kwa ajili ya Taasisi za umma,shughuli za kibiashara pamoja na majumbani, wananchi hao wamepongeza uwepo wa teknolojia hiyo ambayo wamesema licha ya kulinda mazingira lakini pia inarahisisha suala zima la kupika na hivyo kurahisisha maisha.

"Tumefurahi kuona majiko yaliyoboreshwa, teknolojia iliyotumika ni nzuri, majiko haya tumeyapenda,"amesema Fatma Hamis mkazi wa Kiembesamaki.

Suleiman Ally Mkazi wa Masingini Unguja amesema Nishati Safi ya Kupikia inakwenda kupunguza gharama za maisha na amepongeza mkakati wa Serikali katika kuhamasisha matumizi yake.

"Tunatumia gharama kubwa kununua mkaa huu wa kawaida; mimi nitakuwa balozi wa teknolojia hii; Serikali imefanya jambo kubwa muhimu ni kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kama hivi,"amesema Ally.
Akizungumzia kwa ujumla mwenendo wa kuhama kutoka kutumia Nishati chafu ya kupikia kuingia katika Nishati Safi ya Kupikia, Ally anasema si jambo rahisi kubadilisha mazoea ya mtu ila kwa hamasa inayoendelea kutolewa mabadiliko yanayayotarajiwa yatafikiwa.

"Wakati gesi inaingia wengi tulisita kutumia lakini sasa imekuwa ni kimbilio, uelewa unaongezeka kadri siku zinavyokwenda," amesema Ally.
Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ukiwa umeambatana na watengenezaji wa majiko yanayotumia Nishati Safi ya Kupikia ambayo ni kampuni ya ENVOTEC Services Ltd wanashiriki Tamasha la Kizimkazi, katika eneo la Kizimkazi Dimbani Mkoa wa Kusini Unguja Zanzibar kwa lengo la kutoa elimu kuhusu nishati safi ya kupikia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news