Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali yashiriki kikao cha kuwasilishwa Miswada ya Sheria

DODOMA-Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeshiriki kikao cha kuwasilishwa kwa Miswada ya Sheria.
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Pindi Chana akiteta jambo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Feleshi katika kikao hicho cha kuwasilishwa kwa Miswada ya Sheria leo Agosti 14,2024 jijini Dodoma.
Miswada iliyowasilishwa mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria ni pomoja na Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Shule ya Sheria Tanzania, Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali ya mwaka 2024, na Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali Na 2 wa mwaka 2024.
Kikao hicho cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kimefanyika tarehe 14 Agosti 2024 Bungeni Jijini Dodoma.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news