DODOMA-Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kutumia fursa ya Maonesho ya Nanenane yanayoendelea Kitaifa mkoani Dodoma kutoa elimu kwa wadau mbalimbali wanaotembelea banda la chuo katika maonesho haya.

Tunawakaribisha watu wote kuja kusikiliza huduma zitolewazo na chuo na pia kujiunga na chuo hiki, katika maonesho hayo kuna wafanyakazi wa taasisi mbalimbali ambao wako maofisini na wangependa kujiendeleza kielimu wakiwa makazini hivyo chuo kipo hapa kuwasaidia kujiendeleza bila kuvuruga ratiba zao.
Naye Mkurugenzi wa OUT Kituo cha mkoa wa Dodoma Bw. Mohamed Msoroka, ameongeza kuwa tupo Katika maonesho haya kurahisisha kuwafikishia huduma jamii badala ya wateja kutufuata ofisini. Aidha, amewahimiza kutembelea banda la chuo kwa wingi ili kupata huduma za udahili, usajili na ushauri kuhusu programu mbalimbali zitolewazo na chuo.