Pamba Jiji FC, Tanzania Prisons zatoka suluhu mechi ya Ligi Kuu ya NBC

NA DIRAMAKINI

PAZIA la Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara kwa msimu wa 2024/2025 limefunguliwa rasmi kwa kuzikutanisha timu ya Pamba Jiji FC na Tanzania Prisons.
Mtanange huo umepigwa Agosti 16,2024 katika dimba la CCM Kirumba lililopo jijini Mwanza ambapo dakika tisini zimetamatika kwa wawili hao kutoka suluhu ya bila kufungana.

Ikumbukwe kuwa,Pamba Jiji FC imerejea Ligi Kuu NBC Tanzania Bara na kucheza mchezo wake wa kwanza,baada ya takribani miaka 23 kupitia tangu kushiriki ligi hiyo.

Aidha,jumla ya michezo 240 itachezwa sawa na michezo 30 kwa kila timu 16 zinazoshiriki Ligi Kuu ya NBC.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news